• HABARI MPYA

  Thursday, January 05, 2017

  DIAMOND KUTUMBIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA LEO ABUJA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR E SALAAM
  MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wengine wakubwa barani, wanatarajiwa kutumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano mjini Abuja, Nigeria.
  Diamond anaweka rekodi nyingine kubwa katika historia yake ya muziki kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kutumbuiza kwenhye tuzom hizo kubwa barani. 
  Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund ya Ujerumani atatetea tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika dhidi ya Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City na Sadio Mane wa Senegal na Liverpool.
  Diamond Platnumz anatumbuiza usiku wa leo katika sherehe za tuzo Mwanasoka Bora Afrika mjini Abuja, Nigeria

  Miongoni mwa wanamuziki hao, ni mtoto gwiji wa muziki Afrika, Fela-Anikulapo Kuti, aitwaye Femi Kuti. 
  Kuti, ambaye alianzisha bendi yake mwenyewe ya Positive Force mwaka 1986 anafahamika kwa muziki wake mzuri. 
  Amejitambulisha kama gwiji kweli Afro Beat kwa staili yake mwenyewe na moja ya nyimbo zake zinazobamba ni Beng, Beng, Beng.
  Msanii mwingine anayetarajiwa kutumbuiza usiku wa leo ni dansa, mwandishi wa nyimbo na mtumbuizaji, Chinedu Okoli, maarufu Flavour N’abania wa Nigeria. 
  Flavour anafahamika barani na nchi nyingine duniani kwa kibao chake cha kuwarusha watu ‘klabu’ kiitwacho Nwa Baby. 
  Pia watakuwepo Diamond Platinumz mkali wa Bongo Flava kutoka Tanzania ambaye anatamba na kibao chake Salome kwa sasa.
  Wengine ni Omawumi anayetamba na nyimbo za Megbele na If you ask Me, kundi la Muffinz kutoka Afrika Kusini, Yemi Alade na DJ Jimmy Jatt.
  Wakati huo huo; Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou aliwasili mjini Abuja jana na kupokewa na Makamu wake wa kwanza, Almamy Kabele Camara; Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Adoum Djibrine, Rais wa Shirikkisho la Soka Nigeria, Amaju Pinnick na Maofisa mbalimbali wa Globacom, wadhamini wa tuzo shughuli hiyo.

  Pierre-Emerick Aubameyang anatetea tuzo yake dhidi ya Riyad Mahrez na Sadio Mane

  TATU BORA YA TUZO MBALIMBALI LEO
  Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika
  Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
  Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
  Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
  Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika
  Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
  Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)
  Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe)
  Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Kike
  Asisat Oshoala (Nigeria & Arsenal Ladies)
  Elizabeth Addo (Ghana & Kvarnsvedensik)
  Gabrielle Aboudi Onguene (Cameroon & Rossyanka)
  Mwanasoka Bora Anayechipukia
  Elia Meschak (Dr Congo & Tp Mazembe)   
  Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)
  Naby Keita (Guinea & Rb Leipzig)
  Mwanasoka Bora Kijana wa Mwaka
  Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal)
  Eric Ayiah (Ghana And Charity Fc)        
  Sandra Owusu-Ansah (Ghana And Supreme Ladies)
  Kocha Bora wa Mwaka
  Florent Ibenge (Timu ya taifa DRC)
  Pitso Mosimane (Mamelodi Sundowns) 
  Florence Omagbemi (Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria)
  Klabu Bora ya Mwaka
  Mamelodi Sundowns 
  Tp Mazembe     
  Zesco United
  Timu Bora ya Taifa ya Mwaka
  DRC
  Senegal 
  Uganda
  Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka
  Cameroon
  Nigeria  
  Afrika Kusini
  Refa Bora wa Mwaka
  Bakary Papa Gassama      
  Ghead Zaglol Grisha     
  Malang Diedhiou            
  Kiongozi Bora wa Soka wa Mwaka
  Manuel Lopes Nascimento
  Rais wa Shirikisho la Soka Guinea Bissau
  Tuzo ya Gwiji
  Laurent Pokou, mchezaji wa zamani wa Ivory Coast
  Emilienne Mbango, mchezaji wa zamani wa Cameroon

  Kipa Denis Onyango wa Uganda anawania Tuzo ya mchezaji Bora Anayecheza Afrika, baada ya kuipa Mamelodi Sundowns taji la Ligi ya Mabingwa

  Kikosi Bora wachezaji 11
  Kipa: Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns) 
  Mabeki: Serge Aurier (Ivory Coast na Paris Saint-Germain), Aymen Abdennour (Tunisia na Valencia), Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester United), Joyce Lomalisa (DRC na As Vita)
  Viungo: Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns), Rainford Kalaba (Zambia & Tp Mazembe), Keegan Dolly (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns),
  Washambuliaji: Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City) 
  Wa akiba;
  Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile Du Sahel), Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli), Salif Coulibaly (Mali & Tp Mazembe), Islam Slimani (Algeria & Leicester City), Mohamed Salah (Misri & Roma), Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City), Alex Iwobi (Nigeria And Arsenal)

  Samuel Eto'o wa Cameroon anashikilia rekodi ya kushinda tuzo nyingi za Mwanasoka Bora Afrika 

  WALIOWAHI KUWA WANASOKA BORA AFRIKA
  1992 Abedi Ayew Pele (Ghana)
  1993 Rashidi Yekini (Nigeria)
  1994 Emmanuel Amunike (Nigeria)
  1995 George Weah (Liberia)
  1996 Nwankwo Kanu (Nigeria)
  1997 Victor Ikpeba (Nigeria)
  1998 Mustapha Hadji (Morocco)
  1999 Nwankwo Kanu (Nigeria)
  2000 Patrick Mboma (Cameroon)
  2001 El-Hadji Diouf (Senegal)
  2002 El Hadji Diouf (Senegal)
  2003 Samuel Eto'o (Cameroon)
  2004 Samuel Eto'o (Cameroon)
  2005 Samuel Eto'o (Cameroon)
  2006 Didier Drogba (Ivory Coast)
  2007 Frederic Kanoute (Mali)
  2008 Emmanuel Adebayor (Togo)
  2009 Didier Drogba (Ivory Coast)
  2010 Samuel Eto'o (Cameroon)
  2011 Yaya Toure (Ivory Coast)
  2012 Yaya Toure (Ivory Coast)
  2013 Yaya Toure (Ivory Coast)
  2014 Yaya Toure (Ivory Coast)
  2015 Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)
  2016  ?????
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIAMOND KUTUMBIZA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA LEO ABUJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top