TIMU ya Afrika Kusini imefanikiwa kwenda Hatua ya 32 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini katika mchezo wa Kundi A Alfajiri ya leo Uwanja wa BBVA mjini Guadalupe, Nuevo León nchini Mexico.
Shujaa aliyeivusha Bafana Bafana hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika histora yake ya ushiriki wa fainali hizo ni mshambuliaji wa klabu bingwa ya Afrika, Mamelodi Sundowns, Thapelo Maseko aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 63.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, wenyeji Mexico walifuzu Hatua ya 32 Bora kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech Alfajiri ya leo Uwanja wa Azteca Jijini Mexico City.
Mabao ya Mexico yamefungwa na beki wa kushoto wa AZ Alkmaar ya Uholanzi, Mateo Chávez García dakika ya 55, winga wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, Julián Andrés Quiñones Quinones mzaliwa wa Colombia dakika ya 61 na kiungo wa Real Betis ya Hispania, Álvaro Fidalgo Fernández mzaliwa wa Hispania dakika ya 90’+4.
Kwa matokeo hayo, Mexico inamaliza kileleni na pointi zake tisa ikifuatiwa na Afrika Kusini pointi nne n azote zinasonga mbele, huku Korea Kusini iliyomaliza na pointi tatu na Jamhuri ya Czech iliyomaliza na pointi moja safari zao zinaishia hapo.



.png)
0 comments:
Post a Comment