• HABARI MPYA

    Monday, June 15, 2026

    SWEDEN YAANZA NA MOTO KOMBE LA DUNIA, YAIBAMIZA TUNISIA 5-1


    TIMU ya Sweden imeiadhibu vikali Tunisia kwa kuitandika mabao 5-1 Alfajiri ya leo katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa BBVA, Guadalupe, Nuevo León, Kaskazini mwa Mexico.
    Mabao ya Sweden yamefungwa na kiungo wa Brighton & Hove Albion, Yasin Abbas Ayari mwenye asili ya Tunisia na Morocco mawili dakika ya saba na 90’+6, washambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak mwenye asili ya Eritrea dakika ya 30, Viktor Einar Gyökeres wa Arsenal ya England dakika ya 59 na kiungo wa b VfL Wolfsburg ya Ujerumani, Mattias Olof Svanberg dakika ya 84.
    Bao pekee la Tunisia limefungwa na beki wa kati wa Maribor ya Slovenia, Omar Rekik mzaliwa wa Uholanzi, nchi ya mama yake dakika ya 43.
    Ikumbukwe mchezo wa kwanza wa kundi hilo jana Uholanzi ilitoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Japan Uwanja wa AT&T Jijini Arlington, Tarrant County, Texas, Marekani.
    Mabao ya Uholanzi yote yalifungwa na nyota wake wanaocheza England, beki wa Liverpool, Virgil van Dijk dakika ya 50 na winga wa West Ham United, Crysencio Jilbert Sylverio Cirro Summerville dakika ya 64, wakati ya Japan yalifungwa na mshambuliaji wa Reims ya Ufaransa, Keito Nakamura dakika ya 57 na kiungo wa Crystal Palace ya England, Daichi Kamada dakika ya 88.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SWEDEN YAANZA NA MOTO KOMBE LA DUNIA, YAIBAMIZA TUNISIA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top