• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2026

    QATAR YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE 1-1 NA USWISI


    BAO la kujifunga la dakika ya 90’+4 la kiungo wa Hamburger SV ya Ujerumani, Miro Max Maria Muheim liliisaidia Qatar kupata sare ya 1-1 na Uswisi katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Dunia usiku wa Jumamosi Uwanja wa Levi's Jijini Santa Clara, Santa Clara County, California, Marekani.
    Uswisi waliuanza vyema mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza mapema kupitia kwa mshambuliaji wa Rennes ya Ufaransa, Breel Donald Embolo aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 17.
    Ikumbukwe mechi nyingine ya kwanza ya kundi B, wenyeji, Canada nao walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Bosnia & Herzegovina usiku wa juzi Uwanja wa BMO Field, Toronto nchini Canada.
    Mshambuliaji wa Universitatea Cluj ya Romania, Jovo Lukić mzaliwa wa Serbia alianza kuifungia Bosnia & Herzegovina dakika ya 21, kabla ya winga wa Mallorca ya Hispania, Cyle Christopher Larin kuisawazishia Canada dakika ya 78.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: QATAR YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE 1-1 NA USWISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top