• HABARI MPYA

    Wednesday, June 24, 2026

    ENGLAND YAKWAA KISIKI KWA GHANA, ZATOKA SULUHU 0-0 FOXBOROUGH



    TIMU ya England imelazimishwa sare ya bila mabao na Ghana katika mchezo wa Kundi L Fainali za Kombe la Dunia usiku wa jana Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Massachusetts, Marekani.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo usiku wa kuamkia leo bao la dakika ya 54 la mshambuliaji wa Osasuna ya Hispania, Ante Budimir (34) mzaliwa wa Bosnia & Herzegovina liliipa Croatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama Uwanja wa BMO Field, Toronto nchini Canada.
    Msimamo wa Kundi L sasa ni England inaongoza kwa pointi zake nne ikiizidi wastani wa mabao tu Ghana, wakati Croatia inafuatia nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, huku Panama ambayo haina pointi inashika mkia baada ya mechi mbili za mwanzo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENGLAND YAKWAA KISIKI KWA GHANA, ZATOKA SULUHU 0-0 FOXBOROUGH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top