• HABARI MPYA

    Tuesday, June 30, 2026

    MOROCCO YAITOA UHOLANZI KWA PENALTI NA KUTINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Morocco imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa penalty 3-2 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na Uholanzi Asubuhi ya leo Uwanja wa BBVA mjini Guadalupe, jimbo la Nuevo León Kaskazini mwa Mexico.
    Mshambuliaji wa Liverpool ya England, Cody Mathes Gakpo ambaye baba yake ni mwenye asili ya Ghana alizaliwa – alianza kuifungia Uholanzi dakika ya 72, kabla ya beki wa kati wa Fulham ya England pia, Issa Laye Lucas Jean Diop mzaliwa wa Ufaransa ambaye baba yake ni Msenegal kuisawazishia dakika ya 90’+1.
    Katika mikwaju ya penalti walioifungia Morocco ni football Rahimi, Talbi na Saibari huku El Aynaoui na Hakimi wakikosa, wakati kwa upande wa Uholanzi waliofunga ni Koopmeiners na Weghorst pekee huku Kluivert, Timber na Summerville wakikosa nao. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOROCCO YAITOA UHOLANZI KWA PENALTI NA KUTINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top