• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2026

    LUIS DIAZ AFUNGA COLOMBIA YAICHAPA UZBEKISTAN 3-1 MEXICO


    TIMU ya Colombia imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uzbekistan katika mchezo wa Kundi K Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Azteca, Mexico City nchini Mexico.
    Mabao ya Colombia yamefungwa na beki wa kulia wa Crystal Palace ya England, Daniel Munoz Mejía dakika ya 40, viungo, Luis Fernando Díaz Marulanda wa Bayern Munich ya Ujerumani dakika ya 65 na Jaminton Leandro Campaz wa Rosario Central ya Argentina dakika ya 90’+9.
    Kwa upande wao, Uzbekistan bao lao pekee na la kufutia machozi limefungwa na winga wa klabu ya club İstanbul Başakşehir ya nchini Uturuki, Abbosbek Saidzhon ugli Fayzullaev dakika ya 60. 
    Mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia jana, Ureno ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa NRG, Houston, Texas, Marekani.
    Kiungo Paris Saint-Germain ya Ufaransa, João Pedro Gonçalves Neves alianza kuifungia Ureno dakika ya sita, kabla ya winga wa Newcastle United mzaliwa wa Ufaransa, Yoane Wissa kuisawazishia DRC dakika ya 45’+5.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LUIS DIAZ AFUNGA COLOMBIA YAICHAPA UZBEKISTAN 3-1 MEXICO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top