• HABARI MPYA

    Saturday, June 20, 2026

    CUNHA WA MAN UNITED APIGA MBILLI BRAZIL YAICHAPA HAITI 3-0


    TIMU ya Brazil imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Haiti katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Marekani.
    Mabao ya Brazil yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Manchester United ya England, Matheus Santos Carneiro da Cunha mawili dakika ya 23 na 36 na mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior dakika ya 45’+3.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Morocco imeichapa Scotland 1-0, bao la S kiungo mshambuliaji wa PSV Eindhoven, Ismael Saibari mzaliwa wa Hispania aliyekulia Ubelgiji dakika ya pili tu usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Gillette, Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani.
    Msimamo wa Kundi C sasa baada ya kila timu kucheza mechi mbili ni Brazil inaongoza kwa pointi zake nne, ikiizidi tu wastani wa mabao Morocco, huku Scotland ikishukia nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu mbele ya Haiti ambayo haijavuna hata pointi moja hadi sasa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CUNHA WA MAN UNITED APIGA MBILLI BRAZIL YAICHAPA HAITI 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top