WENYEJI, Canada wameibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Qatar katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa BC Place, Vancouver nchini Canada.
Cyle Christopher Larin wa Southampton ya England mwenye asili ya Jamaica dakika ya 16, kabla ya mshambuliaji mwenzake, Jonathan Christian David wa Juventus ya Italia mwenye asili ya Haiti kupiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za 29, 45’+3 na 90’+2.
Mabao mengine ya Canada yamefungwa na kiungo wa Anderlecht ya Ubelgiji, Nathan-Dylan Saliba dakika ya 64 na kiungo wa ulinzi, Mohamed Naceur Manai anayecheza kwa mkopo Al-Shamal kutoka Al-Sadd zote za nyumbani,Qatar aliyejifunga dakika ya 75.
Kwa ushindi huo, Canada inafikisha pointi nne na kupanda kileleni mwa Kundi B ikiizidi tu wastani wa mabao Uswisi inayofuatia nafasi ya pili – huku Bosnia & Herzegovina na Qatar zikifuatia nafasi ya tatu na nne kwa pointi zao moja moja kufuatia timu zote kucheza mechi mbili.
Ikumbukwe jana usiku Uswisi iliichapa Bosnia & Herzegovina mabao 4-1 katika mchezo mwingine wa kundi hilo Uwanja wa SoFi, Inglewood, Los Angeles County, California, .Marekani
Mabao ya Uswisi yalifungwa na viungo, Johan Manzambi wa Freiburg ya Ujerumani, mzaliwa Geneva kwa wazazi kutoka Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mawili dakika ya 74 na 90, Rubén Estephan Vargas Martínez wa Sevilla ya Hispania dakika ya 84 na Nahodha, kiungo wa ulinzi, Granit Xhaka wa Sunderland ya England dakika ya 90’+7 kwa penalti.
Bao pekee la ya Bosnia & Herzegovina lilifungwa na kiungo wa Slovan Liberec ya Jamhuri ya Czech, Ermin Mahmić dakika ya 90’+3.



.png)
0 comments:
Post a Comment