• HABARI MPYA

    Wednesday, June 24, 2026

    MKONGWE ANTE BUDIMIR AFUNGA BAO PEKEE CROATIA YAICHAPA PANAMA 1-0


    TIMU ya Croatia imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama katika mchezo wa Kundi L Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo wa BMO Field, Toronto nchini Canada.
    Bao pekee la Croatia limetumbukizwa nyavuni na mshambuliaji wa Osasuna ya Hispania, Ante Budimir (34) mzaliwa wa Bosnia & Herzegovina aliyefunga dakika ya 54 la.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia usiku wa jana, England ililazimishwa sare ya bila mabao na Ghana Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Massachusetts, Marekani.
    Kwa matokeo hayo, England inaongoza Kundi L kwa pointi zake nne ikiizidi wastani wa mabao tu Ghana, wakati Croatia inafuatia nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, huku Panama ambayo haina pointi inashika mkia baada ya mechi mbili za mwanzo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKONGWE ANTE BUDIMIR AFUNGA BAO PEKEE CROATIA YAICHAPA PANAMA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top