TIMU ya Algeria imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jordan katika mchezo wa Kundi J Fainali za Kombe la Dunia Asubuhi ya leo Uwanja wa Levi's, Santa Clara, California, Marekani.
Mabao ya Algeria yamefungwa na washambuliaji Ahmed Nadhir Benbouali wa Győr ya Hungary dakika ya 69 na Amine Ferid Gouiri wa Marseille ya Ufaransa alikozaliwa dakika ya 82.
Algeria ilipata mabao yakr baada ya kutanguliwa na Jordan ambao bao lao hilo pekee alifunga kiungo wa ulinzi wa Qatar SC ya Qatar, Nizar Mahmoud Ahmed Al-Rashdan dakika ya 36.
Kwa ushindi huo, Algeria inafikisha pointi tatu, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Austria na wote wapo nyuma ya vinara, Argentina wenye pointi sita, wakati Jordan inashika mkia ikiwa haina na pointi baada ya mechi mbili za mwanzo.



.png)
0 comments:
Post a Comment