• HABARI MPYA

    Tuesday, June 16, 2026

    NAMUNGO FC YAAMBULIA SULUHU KWA TRA UNITED, 0-0 RUANGWA


    TIMU ya Namungo FC imelazimishwa sare ya bila mabao na TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
    Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya 11, wakati TRA United inafikisha pointi 41, ingawa inabaki nafasi ya tano baada ya timu zote kucheza mechi 27 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC YAAMBULIA SULUHU KWA TRA UNITED, 0-0 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top