UHOLANZI imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Japan katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Dunia usiku wa Jumapili Uwanja wa AT&T Jijini Arlington, Tarrant County, Texas, Marekani.
Mabao ya Uholanzi yote yalifungwa na nyota wake wanaocheza England, beki wa Liverpool, Virgil van Dijk dakika ya 50 na winga wa West Ham United, Crysencio Jilbert Sylverio Cirro Summerville dakika ya 64, wakati ya Japan yalifungwa na mshambuliaji wa Reims ya Ufaransa, Keito Nakamura dakika ya 57 na kiungo wa Crystal Palace ya England, Daichi Kamada dakika ya 88.
Mchezo mwingine wa kwanza wa Kundi F unaendelea hivi sasa kati ya Sweden na Tunisia Uwanja wa BBVA, Guadalupe, Nuevo León, Kaskazini mwa Mexico.



.png)
0 comments:
Post a Comment