WENYEJI, Mexico wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Korea Kusini katika mchezo wa Kundi A Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Akron, Zapopan, Jalisco nchini Mexico.
Shujaa wa Mexico Alfajiri ya leo ni beki wa kati, mkongwe wa umri wa miaka 31, Luis Francisco Romo Barrón anayechezea klabu ya Guadalajara ya nyumbani aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 50.
Kwa ushindi huo, Mexico inafikisha poinnti sita na kuendelea kuongoza Kundi A ikifuatia na Korea Kusini yenye pointi tatu na Jamhuri ya Czech yenye pointi moja sawa na Afrika Kusini.
Ikumbukwe mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia jana Afrika Kusini ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Jamhuri ya Czech Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia, Marekani.
Mabao yote leo yalifungwa na viungo wanaocheza ligi za nchini mwao, Michal Sadílek wa Slavia Prague akianza kuifungia Jamhuri ya Czech dakika ya sita, kabla ya Teboho Mokoena wa Mamelodi Sundowns kuisawazishia Afrika Kusini kwa mkwaju wa penalti dakika ya 83.



.png)
0 comments:
Post a Comment