• HABARI MPYA

    Sunday, June 21, 2026

    UJERUMANI YATOKA NYUMA NA KUICHAPA IVORY COAST 2-1 KWA MBINDE


    UJERUMANI imetoka nyuma na kushinda mabao 2–1 dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa BMO Field Jijini Toronto nchini Canada.
    Mabao yote ya Ujerumani yamefungwa na mshambuliaji wa VfB Stuttgart ya kwao, Deniz Undav mwenye asili ya Uturuki dakika ya 68 na 90’+4 baada ya kiungo Franck Yannick Kessié wa Al-Ahli ya Saudi Arabia kuanza kuifungia Ivory Coast dakika ya 30.
    Mchezo mwingine wa Kundi F nana ya Ecuador na Curaçao unaendelea hivi Sasa Uwanja wa Arrowhead, Kansas City, Missouri, Marekani.
    Kwa ushindi huo, Ujerumani inapanda kileleni ikifikisha pointi sita ikiizidi pointi tatu Ivory Coast baada ya timu hizo zote kucheza mechi mbili. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJERUMANI YATOKA NYUMA NA KUICHAPA IVORY COAST 2-1 KWA MBINDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top