TIMU ya taifa ya Morocco imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Scotland katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Gillette, Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani.
Bao pekee la Simba wa Atlasi limefungwa na kiungo mshambuliaji wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Ismael Saibari mzaliwa wa Hispania aliyekulia Ubelgiji dakika ya pili tu ya mchezo huo.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Brazil imeichapa Haiti 3-0, mabao ya Cunha, mawili dakika ya23 na 36 na Vinícius dakika ya 45’+3 Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani.
Msimamo wa Kundi C sasa baada ya kila timu kucheza mechi mbili ni Brazil inaongoza kwa pointi zake nne, ikiizidi tu wastani wa mabao Morocco, huku Scotland ikishukia nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu mbele ya Haiti ambayo haijavuna hata pointi moja hadi sasa.



.png)
0 comments:
Post a Comment