TIMU ya Ufaransa imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Iraq katika mchezo wa Kundi I Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Lincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania nchini Marekani.
Mabao ya Ufaransa yamefungwa na washambuliaji, Kylian Mbappé Lottin wa Real Madrid ya Hispania mwenye asili ya Cameroon aliyefunga mawili dakika ya 14 na 54 na Masour Ousmane Dembélé wa club Paris Saint-Germain ya nyumbani mwenye asili ya Mauritania na Mali aliyefunga dakika ya 66.
Kwa ushindi huo, Ufaransa inafikisha pointi sita za mechi mbili na kuendelea kuongoza Kundi I ikifuatiwa na Norway yenye pointi tatu mechi moja, wakati Senegal iliyocheza mechi moja na Iraq mechi mbili ndio vibonde hawana pointi.
Mchezo mwingine wa Kundi I unaendelea hivi Sasa kati ya Norway na Senegal Uwaja wa MetLife, East Rutherford, New York, Marekani.



.png)
0 comments:
Post a Comment