• HABARI MPYA

    Sunday, June 21, 2026

    CURAÇAO YAKOMAA NA ECUADOR ZATOKA SULUHU KOMBE LA DUNIA


    TIMU za Ecuador na Curaçao zimetoshana nguvu kwa sare ya bila mabao katika mchezo wa Kundi E Fainali za Kombe la Dunia Alfajiri ya leo Uwanja wa Arrowhead, Kansas City, Missouri, Marekani.
    Ikumbukwe mchezo uliotangulia wa Kundi hilo Ujerumani ilitoka nyuma na kushinda mabao 2–1 dhidi ya Ivory Coast Uwanja wa BMO Field Jijini Toronto nchini Canada.
    Mabao yote ya Ujerumani yalifungwa na mshambuliaji wa VfB Stuttgart ya kwao, Deniz Undav mwenye asili ya Uturuki dakika ya 68 na 90’+4 baada ya kiungo Franck Yannick Kessié wa Al-Ahli ya Saudi Arabia kuanza kuifungia Ivory Coast dakika ya 30.
    Kwa matokeo hayo, Ujerumani inafikisha pointi sita kileleni mbele ya Ivory Coast yenye pointi tatu, zikifuatiwa na Ecuador na Curaçao zenye pointi moja kila moja baada ya timu hizo zote kucheza mechi mbili. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CURAÇAO YAKOMAA NA ECUADOR ZATOKA SULUHU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top