TIMU ya Afrika Kusini imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Jamhuri ya Czech katika mchezo wa Kundi A Fainali za Kombe la Dunia usiku huu Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia, Marekani.
Mabao yote leo yamefungwa na viungo wanaocheza ligi za nchini mwao, Michal Sadílek wa Slavia Prague akianza kuifungia Jamhuri ya Czech dakika ya sita, kabla ya Teboho Mokoena wa Mamelodi Sundowns kuisawazishia Afrika Kusini kwa mkwaju wa penalti dakika ya 83.
Kwa matokeo hayo kila timu inaokota pointi ya kwanza katika mchezo wa pili kufuatia kupoteza mechi zao za kwanza za kundi hilo, Afrika Kusini ikifungwa 2-0 na Mexico na Jamhuri ya Czech ikifungwa 2-1 na Korea Kusini.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utafuatia Saa 10:00 Alfajiri kati ya Mexico na Korea Kusini Uwanja wa Akron, Zapopan, Jalisco nchini Mexico.



.png)
0 comments:
Post a Comment