TIMU ya Senegal imefanikiwa kufuzu Hatua ya 32 Kombe la Dunia kama moja ya washindi watatu Bora baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Iraq usiku wa jana katika mchezo wa Kundi I Uwanja wa BMO Field, Toronto nchini Canada.
Mabao ya Simba wa Teranga yalifungwa na nyota wanaocheza England, kiungo Mouhamadou Habib Mbacke Diarra wa Sunderland dakika ya nne, Ismaila Sarr Crystal Palace dakika ya 56, kiungo wa Villarreal ya Hispania, Pape Alassane Gueye mzaliwa wa Ufaransa, mawili dakika ya 59 na 71 na kiungo wa Everton ya England pia, Iliman Cheikh Baroy Ndiaye mzaliwa wa Ufarans anaye dakika ya 82.
Senegal inaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kuwahi kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja wa Fainali za Dunia kihistoria.
Mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi I, Ufaransa iliichapa Norway 4-1 mshambuliaji wa Paris Saint-Germain ya kwao, Masour Ousmane Dembélé mwenye asili ya Mali na Mauritania akipiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za saba, 20 na 32 Uwanja wa Gillette Jijini Foxborough, Massachusetts, Marekani.
Bao lingine la Simba wa Teranga lilifungwa na mchezaji mwingine wa Paris Saint-Germain, kiungo mshambuliaji Désiré Nonka-Maho Doué dakika ya 90’+4 na bao la kufutia machozi la la Norway alifunga kiungo Thelonious ‘Thelo’ Gerard Aasgaard wa Rangers ya Scotland, mzaliwa wa England dakika ya 21.
Kwa matokeo hayo, Ufaransa imeongoza Kundi H kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Norway pointi sita na Senegal pointi tatu n azote zinafuzu Hatua ya 32 Bora, huku Iraq iliyoshika mkia kwa kupoteza mechi zote ikirejea nyumbani.



.png)
0 comments:
Post a Comment