TIMU za Uruguay na Cape Verde zimetoshana nguvu kwa sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Kundi H Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens, Florida, Marekani.
Mabao ya Uruguay yalifungwa na winga wa Sporting CP ya Ureno, Maximiliano Javier ‘Maxi’ Araujo Vilches dakika ya 44 na kiungo mshambuliaji wa Fluminense ya Brazil, Agustín Canobbio Graviz dakika ya 45’+6.
Kwa upande wao, Cape Verde mabao yao yalifungwa na kiungo wa ulinzi, Krasnodar ya Urusi, Kevin Lenini Gonçalves Pereira de Pina dakika ya 21 na winga wa Maccabi Tel Aviv ya Israel, Hélio Sandro Oliveira Alves Varela mzaliwa wa Ureno dakika ya 61.
Mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia jana usiku, Hispania iliichapa Saudi Arabia 4-0 mabao ya Lamine Yamal dakika ya 10, Mikel Oyarzabal dakika ya 21 na 24 na Hassan Al-Tambakti aliyejifunga dakika ya 49 Uwanja wa Mercedes-Benz Stadium, Atlanta, Georgia nchini Marekani.
Msimamo wa Kundi H sasa ni Hispania kileleni kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Uruguay na Cape Verde zenye pointi mbili kila moja, wakati Saudi Arabia yenye pointi moja inashika mkia baada ya mechi mbili mbili za mwanzo.



.png)
0 comments:
Post a Comment