• HABARI MPYA

    Tuesday, June 16, 2026

    SAUDI ARABIA YATOA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA URUGUAY KOMBE LA DUNIA



    TIMU ya Saudi Arabia imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Uruguay usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi G Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa Hard Rock, Miami Gardens, Florida, Marekani.
    Beki wa kati wa Al-Nassr ya nyumbani, Riyadh, Abdulelah Ali Awadh Al-Amri alianza kuifungia Saudi Arabia dakika ya 41, kabla ya winga, au beki wa kushoto, Maximiliano Javier Araújo Vilches wa Sporting CP ya Ureno kuisawazishia Uruguay dakika ya 80.
    Mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Hispania ilitoa suluhu (0-0) na Cape Verde usiku wa jana Uwanja wa Mercedes-Benz Jijini Atlanta, Georgia nchini Marekani.
    Sifa zimuendee kipa mkongwe wa umri wa miaka 40, Josimar José Évora Dias ‘Vozinha’ wa klabu ya Chaves ya Ureno aliyedaka kwa ustadi mkubwa na kuokoa michomo mingi ya hatari kuisaidia Cape Verde kupata suluhu hiyo ikicheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kihistoria. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAUDI ARABIA YATOA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA URUGUAY KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top