TIMU ya Norway imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Iraq katika mchezo wa Kundi I Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Gillette, Foxborough, Norfolk County, Massachusetts, Marekani.
Mabao ya Norway yamefungwa na mshambuliaji wa Manchester City, Erling Braut Haaland mawili, dakika ya 29 na 43, beki wa kati wa Genoa ya Italia, Leo Skiri Ostigarddakika ya 76 na mshambuliaji wa Al-Karma ya kwao, Aymen Hussein Ghadhban Al-Mafraje aliyejifunga dakika ya 90’+6 baada ya kuifungia timu yake, Iraq bao la kufutia machozi dakika ya 39.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Ufaransa ilianza vyema kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal usiku wa jana Uwanja wa MetLife, East Rutherford, New Jersey, New York City, Marekani.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé Lottin mwenye asili ya Cameroon amefunga mabao mawili dakika ya 66 na 90’+6 huku bao lingine la Les Bleus likifungwa na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain ya nyumbani, Paris – Bradley Jean-Manuel Essolisam Addo Barcola mwenye asili ya Togo dakika ya 82.
Bao pekee la Senegal lilifungwa na mshambuliaji mwingine wa Paris Saint-Germain, Ibrahim Mbaye mzaliwa wa Ufaransa na ambaye awali alichezea timu za taifa za vijana nchi hiyo ya Ulaya dakika ya 90’+5.



.png)
0 comments:
Post a Comment