• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2026

    KANE APIGA MBILI, BELLINGHAM NA RASHFORD 'MOJA MOJA' ENGLAND YAILAZA CROATIA 4-2


    TIMU ya England imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia katika mchezo wa Kundi L Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa AT&T Stadium, Arlington, Texas, Marekani.
    Mabao ya Three Lions yamefungwa na Nahodha na mshambuliaji, Harry Edward Kane wa Bayern Munich ya Ujerumani mawili, dakika ya 12 kwa penalti na dakika ya 42, kiungo wa Real Madrid ya Hispania, Jude Victor William Bellingham dakika ya 47 na mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford anayecheza kwa mkopo Barcelona ya Hispania dakika ya 85.
    Kwa upande wao Croatia, mabao yao yamefungwa na kiungo wa Como ya Italia, Martin Baturina mzaliwa wa Uswisi dakika ya 36 na mshambuliaji wa FC Dallas ya Marekani, Petar Musa dakika ya 45+5.
    Mchezo mwingine wa KUndi L uliomalizika hivi karibuni, Ghana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama, bao la kiungo wa Nordsjælland ya Denmark, Caleb Marfo Yirenkyi dakika ya 90’+5 Uwanja wa BMO Field, Toronto nchini Canada.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KANE APIGA MBILI, BELLINGHAM NA RASHFORD 'MOJA MOJA' ENGLAND YAILAZA CROATIA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top