• HABARI MPYA

    Friday, June 26, 2026

    PEPE APIGA MBILI NA KUIPELEKA IVORY COAST 32 BORA KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Ivory Coast usiku wa jana ilifanikiwa kwenda Hatua ya 32 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Curaçao katika mchezo wa mwisho wa Kundi E Uwanja wa Lincoln Financial Field mjini Philadelphia, jimbo la f Pennsylvania nchini Marekani.
    Shujaa wa wa Tembo jana alikuwa ni mshambuliaji wa Villarreal ya Hispania, Nicolas Pépé mzaliwa wa Ufaransa aliyefunga mabao hayo yote mawili dakika ya saba na 64.
    Mchezo mwingine wa Kundi E usiku wa jana, Ecuador iliichapa Ujerumani mabao 2-1 Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, jimbo la New Jersey nchini Marekani pia
    Mabao yote katika mchezo huo yalifungwa na mawinga, Leroy Aziz Sané wa Galatasaray ya Uturuki mwenye asili ya Senegal akianza kuifungia Ujerumani dakika ya pili, kabla ya Nilson David Angulo Ramírez wa Sunderland ya England kuisawazishia Ecuador dakika ya tisa na Gonzalo Jordy Plata Jiménez wa Flamengo ya Brazil kufunga la ushindi 77.
    Kwa matokeo hayo, Ujerumani inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake sita ikiizidi tu wastani wa mabao Ivory Coast n azote zinasonga mbele, wakati Ecuador yenye pointi nne inamaliza nafasi ya tatu nayo inafuzu kama mmoja wa washindi watatu bora, huku Curaçao iliyoshika mkia kwa pointi yake moja safari yake ikiishia hapo.

    TIMU ZILIZOFUZU HATUA YA 32 BORA KOMBE LA DUNIA HADI SASA...

    KundiVinaraWashindi wa piliWashindi wa tatu boraZilizofuzu bila
    kumaliza mechi
    A Mexico South Africa
    B Switzerland Canada Bosnia and Herzegovina
    C Brazil Morocco
    D United States Australia
    E Germany Ivory Coast Ecuador
    F Netherlands Japan Sweden
    G
    H
    I France
     Norway
    J Argentina
    K Colombia
    L
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEPE APIGA MBILI NA KUIPELEKA IVORY COAST 32 BORA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top