TIMU ya Iran imetoa sare ya kufungana bao 2-2 na New Zealand Alfajiri ya leo katika mchezo wa Kundi H Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa SoFi Jijini Inglewood, Los Angeles, California, Marekani.
Mabao ya Iran yalifungwa na beki wa Esteghlal ya nyumbani, Tehran, Ramin Salehrad Rezaeian dakika ya 32 na winga wa Rostov ya Urusi, Mohammad Mohebi dakika ya 64, wakati ya New Zealand yote yalifungwa na winga wa Motherwell ya Scotland, Elijah Henry Just mwenye asili ya Ujerumani kwa baba na China kwa mama dakika ya saba na 54.
Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi H usiku wa jana Ubelgiji ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Misri Uwanja wa Lumen Field Jijini Seattle, Washington, Marekani.
Kiungo Emam Ashour Metwally Abdel Ghany alianza kuifungia Misri dakika ya 19, kabla ya mchezaji mwenzake wa Al Ahly ya nyumbani, Cairo – beki Mohamed Hany Gamal El-Demerdash kujifunga dakika ya 66 katika jitihada za kuokoa na kujiikuta anaipatia Ubelgiji bao la kusawazisha.



.png)
0 comments:
Post a Comment