TIMU ya Ujerumani imeanza kwa kishindo Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Curaçao Jumapili kwenye mchezo wa Kundi E Uwanja wa NRG Jijini Houston, Kusini mwa Marekani.
Mabao ya Ujerumani yamefungwa na kiungo, Felix Kalu Nmecha mwenye asili ya Nigeria dakika ya sita, beki Nico Cédric Schlotterbeck dakika ya 38 wote wa Borussia Dortmund na mshambuliaji wa mabingwa wa England, Arsenal, Kai Lukas Havertz mawili dakika ya 45’+5 kwa penalti na 88.
Mabao mengine ya Ujerumani yamefungwa na kiungo wa Bayern Munich, Jamal Musiala mwenye asili ya Nigeria dakika ya 47, beki wa Eintracht Frankfurt, Nathaniel Christopher Brown mwenye asili ya Marekani dakika ya 68 na mshambuliaji wa VfB Stuttgart, Deniz Undav mwenye asili ya Uturuki dakika ya 78, wakati la Curaçao limefungwa na beki wa FC Zurich ya Uswisi, Livano Shyron Liomar Comenencia mzaliwa wa Uholanzi dakika ya 21.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, Ivory Coast wataikaribisha Ecuador mapema kesho Uwanja wa Lincoln Financial Field Jijini Philadelphia, Marekani.

.png)
0 comments:
Post a Comment