MABINGWA watetezi, Argentina Alfajiri ya leo wameanza vyema Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria katika mchezo wa Kundi J Uwanja wa Arrowhead Stadium, Kansas City, Missouri, Marekani.
Mabao yote ya La Selección yamefungwa na mshambuliaji wa Inter Miami ya Marekani, Lionel Andrés Messi dakika ya 17, 60 na 76 ambaye Juni 24 mwaka huu atatimiza miaka 39 tangu azaliwe huko Rosario, Santa Fe na hiyo ikiwa hat-trick ya kwanza kwenye michuano hiyo aliyoanza kucheza mwaka 2006 nchini Ujerumani
Mchezo mwingine wa Kundi J unaendelea hivi sasa Uwanja wa Levi's, Santa Clara, California, Marekani kati ya Austria na Jordan.



.png)
0 comments:
Post a Comment