TIMU ya Cape Verde imefanikiwa kufuzu Hatua ya 32 Fainali za Kombe la Dunia licha ya sare ya bila kufungana na Saudi Arabia Alfajiri ya leo katika mchezo wa Kundi H Uwanja wa NRG, Houston, Texas nchini Marekani.
Kilichowabeba Cape Verde ni Hispania kuichapa 1-0 Uruguay, bao la kiungo mshambuliaji wa Atlético Madrid ya kwao dakika ya 42 katika mchezo mwingine wa Kundi H Uwanja wa Akron mjini Zapopan nchini Mexico.
Kwa matokeo hayo, Hispania imemaliza kileleni mwa Kundi H na pointi zake tisa ikifuatiwa na Cape Verde iliyomaliza na pointi tatu ilizovuna kwenye sare tupu na zote zinasonga mbele.
Uruguay iliyomaliza na pointi zake mbili sawa na Saudi Arabia zote zinapanda ndege kurejea katika nchi zao baada ya kutupwa nje ya Fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia.



.png)
0 comments:
Post a Comment