• HABARI MPYA

  Sunday, May 07, 2023

  CAF YAILIMA YANGA FAINI DOLA 35,000 NA SHARTI ZITO


  KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeipiga faini dola za Kimarekani 35,000, zaidi ya Shilingi Milioni 80 za Tanzania klabu ya Yanga kwa makosa mawili.
  Taarifa ya CAF imesema kwamba kosa la kwanza ni mashabiki wake kufyatua mafataki wakati wa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria ambalo wametozwa dola 10,000.
  Kosa lingine ni madai ya Rivers kwamba basi lao lilivamiwa kuibiwa fedha dola 5,200 na kupulizwa dawa yenye harufu mbaya, wametozwa dola 25,000. 
  Pamoja na hayo, CAF imeaigiza Yanga baada ya kuingia Nusu Fainali wanatakiwa kusimamia usalama wapinzani wao, Marumo Gallants ya Afrika Kusini wakiwa Tanzania kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.
  Hatua hizi kali za CAF kwa Yanga zinatokana na mfululizo wa taarifa za matukio ya aina hiyo katika mechi zinazochezwa Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAILIMA YANGA FAINI DOLA 35,000 NA SHARTI ZITO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top