VIONGOZI wa Yanga SC wakiongozwa na Rais wa KLABU, Hersi Ally Said leo mchana wameshiriki mazishi ya mtoto wa mchezaji wao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ yaliyofanyika Magomeni, Dar es Salaam.
Mtoto huyo aliyepewa jina Feisal kwa heshima ya kiungo Mzanzibari wa klabu hiyo, Feisal Salum Abdallah amefariki miezi mitatu tu tangu azaliwe.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amin.
0 comments:
Post a Comment