• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 26, 2021

  TAIFA STARS YATUPWA NJE AFCON YA CAMEROON MWAKANI BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA EQUATORIAL GUINEA MJINI MALABO

  TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Equatorial Guinea jana Uwanja wa Nuevo do Malabo.
  Katika mchezo huo wa Kundi D kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani Cameroon, bao pekee la Equatorial Guinea lilifungwa na Nahodha wake, Emilio Nsue Lopez dakika ya 90.
  Sasa Equatorial Guinea inafikisha pointi tisa na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Tunisia zote zikifuzu AFCON ya mwakani. 
  Tanzania inabaki nafasi ya tatu na itamenyana na Libya wiki ijayo Dar es Salaam kukamilisha ratiba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YATUPWA NJE AFCON YA CAMEROON MWAKANI BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA EQUATORIAL GUINEA MJINI MALABO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top