• HABARI MPYA

  Wednesday, March 03, 2021

  JESUS AFUNGA MAWILI MAN CITY YAICHAPA WOLVES 4-1 ETIHAD


  TIMU ya Manchester City imeichapa Wolverhampton Wanderers mabao 4-1 jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad, huo ukiwa ushindi wa 21 mfululizo kwa kikosi cha kocha Mspaniola, Pep Guardiola.
  Mabao ya Manchester City yalifungwa na Leandro Dendoncker aliyejifunga dakika ya 15, Gabriel Jesus mawili dakika za 80 na 90 na ushei na na Riyad Mahrez dakika ya 90, wakati la Wolves lilifungwa na Conor Coady dakika ya 61.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 65 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 15 zaidi ya mahasimu wao, Manchester United ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JESUS AFUNGA MAWILI MAN CITY YAICHAPA WOLVES 4-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top