• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 25, 2021

  UFARANSA YATOA SARE 1-1 NA UKRAINE KUFUZU KOMBE LA DUNIA


  UFARANSA imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ukraine katika mchezo wa kwanza wa Kundi D kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya jana Uwanja wa Stade de France Jijini Paris.
  Mshambuliaji wa Barcelona, Antoine Griezmann alianza kuwafungia mabingwa hao wa dunia dakika ya 19, kabla ya beki wa PSG, Presnel Kimpembe kujifunga dakika ya 57 kuwapatia bao la kusawazisha Ukraine.
  Kwa matokeo hayo, Ufaransa timu hizo zinaungana na Bosnia-Herzegovina na Finland kuanza na pointi moja baada ya nao kutoka sare ya 2-2 jana Uwanja wa Helsingin Jijini Helsinki, wakati Kazakhstan ambayo haijacheza haina pointi
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UFARANSA YATOA SARE 1-1 NA UKRAINE KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top