• HABARI MPYA

  Monday, March 15, 2021

  TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA HARAMBEE SRARS KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO NAIROBI

  WENYEJI, Kenya wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwania wa Nyayo Jijini Nairobi.
  Mshambuliaji Eric Kapaito alianza kuifungia Harambee Stars dakika ya 21, kabla ya kiungo wa Azam FC, Ayoub Lyanga kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 39.
  Lakini beki Abdallah Hassan akawafungia Wakenya bao la ushindi dakika ya 58 katika mchezo huo maalum kwa timu zote kujiandaa na mechi mbili za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Cameroon.


  Timu hizo zitarudiana Alhamisi Saa 1:00 usiku Uwanja wa Kasarani, hapo hapo Nairobi.
  Kikosi cha Kenya kilikuwa; James Saruni, Michael Kibwage, Johnstone Omurwa, Daniel Sakari, Harun Mwale, Kevin Kimani/Elvis Baranga dk62, Kenneth Muguna, Lawrence Juma/, Michael Mutinda/Danson Namasaka dk31, James Mazembe/Abdallah Hassan dk46 na Eric Kapaito.
  Tanzania; Juma Kaseja/Metacha Mnata dk46, Kelvin Yondani, Nickson Kibabage/Yassin Mustapha dk75, Bakari Mwamnuyeto, Israel Mwenda, Salum Abubakar, Himid Mao, Ayoub Lyanga/Kelvin Pius dk84, Feisal Salum/Deus Kaseke dk68, Iddi Nado na Farid Mussa/Abdul Suleiman dk68.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA HARAMBEE SRARS KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI LEO NAIROBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top