• HABARI MPYA

  Wednesday, March 17, 2021

  REAL MADRID YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA


  TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mbingwa Ulaya baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Atalanta kwenye mchezo wa marudiano wa Hatua ya 16 Bora jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano Jijini Madrid.
  Mabao ya Real Madrid jana yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 34 hilo likiwa bao lake la 70 kwenye Ligi ya Mabingwa, Sergio Ramos kwa penalti dakika ya 60 na Marco Asensio dakika ya 84, wakati la Atalanta lilifungwa na Luis Muriel dakika ya 83 na kwa matokeo hayo, Madrid inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Italia
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top