• HABARI MPYA

  Thursday, March 04, 2021

  BARCA YAILAZA SEVILLA 3-0 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MFALME


  Barcelona imefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Mfalme, Ufaransa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Sevilla jana, mabao ya Ousmane Dembele, Gerard Pique na Martin Braithwaite Uwanja wa Camp Nou.
  Kwa matokeo hayo, Barcelona inatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali mwezi Februari.
  Sevilla ilipoteza nafasi nzuri ya kupata bao baada ya mkwaju wa penalti wa Lucas Ocampos kuokolewa na Marc-Andre ter Stegen na sasa Barce itakutana na mshindi kati ya Athletic Bilbao na Levante katika fainali
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCA YAILAZA SEVILLA 3-0 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top