• HABARI MPYA

  Monday, March 22, 2021

  LEICESTER CITY YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  TIMU ya Leicester City imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United Uwanja wa King Power, Leicestershire.
  Mabao ya Leicester yalifungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 24 na 78 na Youri Tielemans dakika ya 52, wakati la Man United lilifungwa na Mason Greenwood dakika ya 38.
  Sasa Laicester City itakutana na Southampton katika Nusu Fainali wakati Chelsea iliyoitoa Sheffield United itakutana na Manchester City iliyoitoa Everton Aprili 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LEICESTER CITY YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top