• HABARI MPYA

  Sunday, March 28, 2021

  TAIFA STARS YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUFUZU AFCON KWA KUICHAPA LIBYA 1-0 BAO PEKEE LA MSUVA

  TANZANIA imekamilisha mechi zake za Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Wydad Club Athletic ya Morocco, Simon Happygod Msuva aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45. 
  Pamoja na ushindi huo, Taifa Stars haijafuzu AFCON kufuatia kuzidiwa kete na Tunisia na Equatorial Guinea zilizoshika nafasi mbili za kwanza na kukata tiketi ya Cameroon mwakani. 
  Tanzania inamaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake saba, nyuma ya Equatorial Guinea yenye pointi tisa, Tunisia pointi 16, wakati Libya yenye pointi tatu imeshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUFUZU AFCON KWA KUICHAPA LIBYA 1-0 BAO PEKEE LA MSUVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top