• HABARI MPYA

  Monday, March 01, 2021

  SIMON MSUVA AFUNGA WYDAD CASABLANCA YAICHAPA KAIZER CHIEFS 4- LIGI YA MABINGWA OUAGADOUGOU

  Na Mwandishi Wetu, OUAGADOUGOU
  NYOTA wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga bao moja, timu yake, Wydad Athletic Club, maarufu kama Wydad Casablanca ikiibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs FC ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika jana Uwanja wa Du 4 Aout Jijini Ouagadougou, Burkina Faso.
  Katika mechi hiyo ambayo Wydad waliikaribisha Kaizer Chiefs Ouagadougou badala ya kwao Casablanca kutokana vipingamizi vya watu wa Afrika Kusini kuingia Morocco kwa sababu ya COVID 19, Msuva alifunga bao la tatu dakika ya 86 akimalizia pasi ya Walid El Karti.
  Mabao mengine ya Wydad yalifungwa na Mohammed Ounajem dakika ya saba, Ayoub El Kaabi dakika ya 44 na Yahya Jabrane kwa penalti dakika ya 90 na ushei.


  Kwa ushindi huo, Wydad inafikisha pointi sita baada ya kushinda mechi zote mbili za mwanzo na sasa inaongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Horoya ya Guinea yenye ponti nne, Kaizer Chiefs pointi moja na Petro de Luanda ya Angola inayoshika mkia kufuatia kufungwa mechi zote mbili za kwanza.
  Mechi nyingine ya Ligi ya Mabingwa jana, Mamelodi Sundowns iliichapa Belouizdad ya Algeria 5-1 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, huo ukiwa mchezo wa Kundi B.
  Sasa Mamelodi Sundowns inaongoza kwa pointi zake sita, ikifuatiwa TP Mazembe ya DRC yenye pointi mbili, Al Hilal ya Sudan pointi moja sawa na Belouizdad baada ya timu zote kucheza mechi mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA AFUNGA WYDAD CASABLANCA YAICHAPA KAIZER CHIEFS 4- LIGI YA MABINGWA OUAGADOUGOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top