• HABARI MPYA

  Thursday, March 11, 2021

  LIVERPOOL WATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA


  MABAO ya Mohamed Salah dakika ya 70 akimalizia pasi ya Diogo Jota na Sadio Mane dakika ya 74 akimalizia pasi ya Divock Origi jana yaliipa Liverpool ushindi wa 2-0 dhidi ya RB Leipzig katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest nchini Hungary.
  Kwa matokeo hayo, Liverpool inatinga Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Februari 16 hapo hapo Budapest, tena hao hao Salah na Mane wakifunga
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL WATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top