• HABARI MPYA

  Sunday, March 21, 2021

  MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Goodison Park, mabao ya Ilkay Gundogan dakika ya 84 na  Kevin De Bruyne dakika ya 90.Nayo Southampton FC iliichapa AFC Bournemouth 3-0, mabao ya viungo wa kimataifa wa Mali, Moussa Djenepo dakika ya 37 na wa England, Nathan Redmond dakika ya 45 na 59 Uwanja wa Vitality.
  Mechi za Nusu Fainali za Kombe la FA England zinatarajiwa kuendelea leo, Chelsea na Sheffield United Saa 10:30 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na Leicester City na Manchester United Saa 2:00 usiku Uwanja wa King Power, Leicestershire 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top