• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 29, 2021

  MBAPPE AKOSA PENALTI, LAKINI UFARANSA YASHINDA 2-0


  PAMOJA na mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappe kukosa penalti dakika ya 75, lakini Ufaransa jana iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kazakhstan mabao ya Ousmane Dembele dakika ya 19 na Sergiy Maliy aliyejifunga dakika ya 44 katika mchezo wa Kundi D kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa Astana Arena mjini Nur-Sultan.
  Mabingwa wa dunia, Ufaransa wanafikisha pointi wanafikisha pointi nne baada ya mechi mbili na kuendelea kuongoza kundi kwa pointi mbili zaidi ya Finland na Ukraine, wakati Bosnia-Herzegovina ina pointi moja na Kazakhstan haina kitu
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBAPPE AKOSA PENALTI, LAKINI UFARANSA YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top