• HABARI MPYA

  Friday, March 05, 2021

  SIMBA QUEENS WAICHAPA YANGA PRINCESS 3-0 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU YA WANAWAKE BARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya wanawake ya Simba, Simba Queens leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya watani wao, Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Queens ambao ni mabingwa watetezi wanapanda kileleni, wakifikisha 39, moja zaidi ya Princess baada ya wote kucheza mechi 15 katika ligi ya timu 12, wakati JKT Queens yenye pointi 36 inabaki nafasi ya tatu.
  Ikiongozwa na kocha Mussa Hassan Mgosi, mchezaji nyota wa zamani wa timu ya wanaume, Simba Queens ilipata mabao yake kupitia kwa Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ dakika ya 30, Opa Clement Sanga dakika ya 43 kwa penalti na Mkongo Joel Bukuru dakika ya 50.
  Yanga Princess inayofundishwa na mchezaji nyota wa zamani wa timu yake ya wanaume, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ ilimaliza pungufu baada ya beki wake, Happyness Mwaipaja kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 43 kufuatia kuzuia mpira kwa mkono kwenye boksi na kusababisha penalti iliyowapa bao la pili wapinzani. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS WAICHAPA YANGA PRINCESS 3-0 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU YA WANAWAKE BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top