• HABARI MPYA

  Friday, March 12, 2021

  MAN UNITED SARE YA 1-1 NA AC MILAN OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na AC Milan katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora UEFA Europa League Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 18, Muivory Coast, Amad Diallo alianza kuifungia Man United dakika ya 50 akimalizia pasi ya Bruno Fernandes, kabla ya beki mkongwe, Mdenmark Simon Thorup Kjaer kuisawazishia AC Milan dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya kiungo Rade Krunic na timu hizo zitarudiana Machi 18 Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED SARE YA 1-1 NA AC MILAN OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top