• HABARI MPYA

  Tuesday, March 16, 2021

  ANTHONY JOSHUA NA TYSON FURY WASAINI MKATABA KUPAMBANA


  MABONDIA Waingereza Anthony Joshua na Tyson Fury wamesaini mkataba wa Pauni Milioni 200 kwa ajili ya pambano la kuunganisha mataji ya uzito wa juu – Promota wa Joshua, Eddie Hearn ametangaza jana.
  Joshua atatetea mataji yake ya WBA, IBF na WBO dhidi ya bingwa wa WBC, Fury katika tarehe itakayotajwa baadaye.
  Joshua amepoteza pambano moja tu kati ya 25 aliyocheza akipigwa na Andy Ruiz Jr Juni mwaka 2019, wakati Fury ana droo moja tu na Deontay Wilder katika mapambano yake 32 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ANTHONY JOSHUA NA TYSON FURY WASAINI MKATABA KUPAMBANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top