• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 12, 2021

  IDDI SULEIMAN 'NADO' APIGA MBILI, AYOUB LYANGA MOJA AZAM FC YAWACHAPA IHEFU SC 3-0 LIGI KUU CHAMAZI

  MABAO ya Iddi Suleiman 'Nado' dakika ya tisa na 90 na Ayoub Lyanga dakika ya 52 jana yaliipa Azam FC ushindi wa 3-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
  Azam FC inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 24, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wana mechi nne mkononi.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu jana, bao pekee la Lusajo Mwaikenda dakika ya 35 liliipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
  KMC inafikisha pointi 35 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 24 pia, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi nne na Biashara United inayshika nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: IDDI SULEIMAN 'NADO' APIGA MBILI, AYOUB LYANGA MOJA AZAM FC YAWACHAPA IHEFU SC 3-0 LIGI KUU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top