• HABARI MPYA

  Tuesday, March 30, 2021

  ALIYELISIFIA BAO LA MORRISON BUNGENI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa nchi.
  Mpango alijipatia umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa michezo baada ya kusifia bao la Mghana Bernard Morrison aliloifungia Yanga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Simba Machi 18 mwaka jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  Dk Mpango alilisifu bao hilo wakati hotuba ya kufungia Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2020-2021 Bungeni Jijini Dodoma Juni mwaka jana.
  Dk Mpango alikumbushia bao hilo siku huyo, huku akiwapiga kijembe kimtindo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndungai na Naibu wake, Dk Tulia Ackson wakati akimwagia sifa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Dk John Magufuli.
  "Mheshimiwa Spika, mwisho,  japo si kwa umuhimu Rais wetu ni mkakamavu na mpezni wa maendeleo ya michezo nchini," alisema Dk Mpango na kuongeza kwenye kufungia hotuba yake kwa kusema; "Mnamfahamu katika ubora wake, mazoezi ya push-ups anazopiga usiige!,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYELISIFIA BAO LA MORRISON BUNGENI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top