• HABARI MPYA

  Sunday, March 07, 2021

  SIMON MSUVA APIGA BAO LA PILI WYDAD CASABLANCA YAICHAPA HOROYA 2-0 LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva jana amefunga bao moja klabu yake, Wydad Casablanca ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Horoya ya Guinea katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.
  Msuva, nyota wa zamani wa klabu ya Yanga ya nyumbani, Tanzania alifunga bao hilo dakika ya 90 akimalizia Ayoub El Kaabi, aliyefunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa pasi ya mshambuliaji mwenzake Mmoroco, Walid El Karti.
  Kwa ushindi huo, Wydad inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi C, ikifuatiwa na Horoya yenye pointi nne sawa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakati Petro Atletico ya Angola inashika mkia ikiwa haina pointi baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMON MSUVA APIGA BAO LA PILI WYDAD CASABLANCA YAICHAPA HOROYA 2-0 LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top