• HABARI MPYA

  Thursday, March 11, 2021

  MAN CITY YAWAPIGA SOUTHAMPTON 5-2 NA KUJIWEKA SAWA KILELENI


  TIMU ya Manchester City jana imeibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad, Manchester.
  Mabao ya Man City yalifungwa na Kelvin De Bruyne mawili dakika ya 15 na 59, Riyad Mahrez mawili dakika ya 40 na 55 na Ilkay Gündogan dakika ya 45, wakati ya Southampton yalifungwa na James Ward-Prowse kwa penalti dakika ya 25 na Che Adams dakika ya 56.
  Man City wanafikisha pointi 68 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 29 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 14 zaidi ya Manchester United wanaofuatia ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi
     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAWAPIGA SOUTHAMPTON 5-2 NA KUJIWEKA SAWA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top